Thursday, 20 February 2014

TANZANIA YATANGAZA KUSHIRIKI MAONYESHO YA 53 YA KIMATAIFA YA MADINI YA VITO NA USONARA NCHINI THAILAND.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7AifkZ_Dv7iVq-PlqJJOhX-T-1JRWPQyDcFJkWyeopO_G9MTBBrZPzVFEXgjEtcHw-P15T91LSrg1x6-n4qTc-PbOyXU0ZY5bRweka7AGEjWE1U3uzirgxWdInBDCoNQ-Hy484wlWOn11/s1600/unnamed+(54).jpg 

Kutokana na Tanzania kuwa na Hazina kubwa ya Madini ya aina mbalimbali inatarajiwa kushiriki maonyesho ya Madini ya Vito na Usonara ikiwa ni miongoni mwa nchi 150 zinazotegemewa kushiriki ,Maonyesho ya 53  ya Kimataifa  yanayojulikana kama ''Bangkok Gems and Jewelry fair''   yatakayofanyika kuanzia tarehe 25 February hadi Tarehe 1 Machi,2014 Bangkok Thailand.

Akizungumzia ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo jana,Kamishna wa Madini,Mhandisi Paul Masanja alieleza kuwa ,Tanzania inatarajia kuyatumia maonyesho hayo kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Thailand katika biashara ya Vito na Usonara,Kutangaza madini ya Vito yanayopatikana nchini kwenu na pia kutafuta masoko mapya biashara.

No comments: