Mgeni Rasmi, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter
Muhongo akihutubia wageni rasmi (hawapo pichani) waliohudhuria hafla ya
uzinduzi wa AWANGO uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency,jijini Dar es
salaam,usiku wa jana.Waziri Muhongo aliwapongeza TOTAL kwa juhudi
wanazozifanya kusaidia jamiii ya
watanzania kupata chnzo cha Nishati kitakachowaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Pembeni ni baadhi ya bidhaa hizo zinazotumia nishati ya jua.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
(kulia),Mgeni rasmi katika uzinduzi wa bidhaa zinazotumia Nishati ya jua
kuzalisha umeme zinazojulikana kama
AWANGO,wa kwanza kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini nTanzania Mh Marcel
Escure pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TOTAL nchini Tanzania Bw.Stephane Gay
wakishuhudia tukio mojawapo katika hafla hiyo.
Meneja wa Maswala ya Kisheria Bi Marsha Msuya akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa AWANGO zilizo chini ya mradi wa TOTAL unaojulikana kama ‘’Total
Access to Solar’’ (TATS) wenye lengo la
kutatua tatizo la ukosefu wa umeme nchini Tanzania kwa jamii ya watu wa kipato
cha chini wakiwa na malengo ya kuhakikisha bidhaa hizo zinafika mikoa yote ya
nchi nzima.
Source: Michuzi Blog.
No comments:
Post a Comment