Mzee Jumanne Mhero Ngoma (Mvumbuzi wa Madini Pekee duniani
yanayopatikana nchini Tanzania)
Historia ya Mvumbuzi
Jumanne
Mhero Ngoma, Mtoto Wa Mfugaji. Alizaliwa Katika Kijiji Cha Marwa, Wilaya Same
Mkoa Wa Kilimanjaro, Wazazi Wake Walihamia Mererani Wakitokea Kijiji Cha Marwa Kwa Ajili
Ya Kutafuta Malisho Ya Mifugo Yetu.
Alipokuwa
Mdogo, Alikuwa Akimsaidia Baba Yake Kuchunga Mifugo Yao Wakati Wa Likizo.
Kama
Ilivyo Kawaida Kwa Watoto Wadogo Kupenda Kucheza, Nilipokuwa Porini Nilikuwa
Nachezea Mawe Ambayo Yalinivutia Kwa Rangi Zake, alikuwa akiyapanga kutokana
Uwepo Wa Rangi Zake Tofauti Na Kuyapa Majina Ya Mifugo yao. Sehemu Hasa
Niliyokuwa Nayapata Mawe Haya Inajulikana Kama Kijiji Cha Nyaisunyae.
Mzee Ngoma
alipata Elimu Yangu Ya Awali Town School Iliyopo Mkoani Arusha Na Kufaulu
Kujiunga Mringa Middle School Mkoani Arusha Ambapo hakubahatika Kumaliza
Kutokana Na Kufariki Baba Yangu Na Kukosa Mtu Wa kumlipia Ada.
Baada
Ya Kushindwa Kuendelea Na Elimu Yangu Ya Middle School Nilirudi Pale Mererani
Kuendelea Kuchunga Mifugo Ya Baba yake Japo Nilikuwa Bado Na Mwamko Na Ari Wa
Kuendelea Na Kupata Elimu.
Mwaka
1966 aliabahatika Kwenda Kusoma Morogoro Chuo Cha Madini Kwa Muda Wa Miezi
Mitatu, Baada Ya Kupata Msaada Wa Kaka yake Ambaye Wakati Huo Nae Alikuwa
Akifanya Kazi Ya Udereva. Alipokuwa Chuoni Chini Ya Mwalimu wake Aliyekuwa Akiitwa
Mkali Dachi Alimsaidia Sana Kupata
Utaalam Wa Mambo Ya Madini. Mara Baada
Ya Kumaliza Chuo Na Kupata Elimu Ya Madini, June 1966, Alibahatika Kupata
Leseni yake Ya Uchimbaji Wa Madini, Alirudi
Mererani, alipofika Mererani aliamua Kuchukua Yale Mawe Ambayo Nilikuwa anachezea
Japo Yalikuwa Tofauti Sana Na Aina Ya Madini aliyofundishwa Pale Morogoro, Aliamua
Kuyachukua Na Kuyapeleka Moshi Office Ya
Madini Wakati Huo Mwanzoni Mwa Mwaka 1967 Ili Yaweze Kufanyiwa Utafiti Kuwa
Yalikuwa Mawe Gani. alibahatika Kuonana Na Afisa Wa Madini Bwana Bills. Kwa
Bahati Mbaya Nae Alishindwa Kuyatambua Japo Yalimvutia Sana Na Kujaribu
Kuyafananisha Na Madini Ya Blue Tourmaline Baada Ya Majadiliano
Nae walikubaliana Ayapeleke Office Madini Dodoma Kwa Utafiti Zaidi.
Baada
Ya Uchunguzi Wa Maabara Ya Madini Dodoma, Mnamo Septemba 1967 Majibu Yalitoka
Na Kuonyesha Kuwa Ni Madini Jamii Ya Zoisite, Na Kushauri Kuwa Kwa Kipindi
Hicho Hayakuwa Na Soko Japo Soko Linaweza Kuwepo Baadae.
Uchunguzi Mwingine Zaidi
Uliohusisha Ofisi Nyingine Za Serikali Ambapo Mwaka 1984, Pro. Simon Mbilinyi Mshauri Wa Uchumi
Ofisi Ya Rais Kipindi Hicho, Alithibitisha Kuwa Mgunduzi Wa Madini Ya Tanzanite
Ni Bwana Jumanne Mhero Ngoma. Rais Alikubali Kwa Maandishi Akaamuru
Apewe Tuzo Na Cheti Cha Utambuzi
……………………..Endelea
Kufuatilia, historia yake inaendelea………………………..
1 comment:
God bless you Mr ngoma
Post a Comment