Waziri wa Nishati na Madini,
Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akiongea na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini
uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
------------------------------------------
Jamhuri ya Muungano Tanzania
kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetenga jumla ya shilingi bilioni 8.9 kwa ajili
kuwainua wachimbaji wadogo wa madini nchini
ili kuwawezesha katika shughuli
zao za uchimbaji wa madini.
Serikali katika jitihada za kuwainua wachimbaji wadogo
zinalenga pia kuinua pato la taifa kutokana na kuongezeka kiwango cha kodi na
tozo mbalimbali zinazopaswa kulipwa na wachimbaji hao kwa serikali.
Akizungumza na wajumbe
waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini nchini,
uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni,
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo alisema
“Tunayo dhamira ya dhati
kuwasaidia ili maisha yenu yaboreke na pia ili kukuza pato la taifa hili”,
alisisitiza Waziri Muhongo na kuongeza kuwa Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) ndilo limepewa jukumu la kusimamia mipango ya uendelezaji wachimbaji
wadogo kwa kushirikiana na taasisi nyingine mbalimbali zinazohusika na sekta ya
madini.
Ili kufanisha zoezi hili Profesa Muhongo amewataka wachimbaji wadogo wa
madini nchini kuhakikisha wanasajili biashara zao, kuanisha mapato yao, pamoja
na kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazowahusu ili taifa liweze kunufaika na
rasilimali hiyo ya madini.
No comments:
Post a Comment