Thursday, 19 December 2013

WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA (TMAA) YAKUSANYA MABILIONI YA KODI

Kampuni zinazomiliki migodi mikubwa na ya kati nchini zimeendelea kulipa stahiki mbalimbali za Serikali, ikiwa ni pamoja na kodi ya mapato.
Katika kuonyesha kwa vitendo, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imetoa rekodi inayoonyesha walivyolipa kodi katika kipindi cha Mei hadi Novemba 2013.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (TMAA), Dk Yamungu Kayandabila   anasema Kampuni ya Resolute Tanzania inayomilikiwa na mgodi wa dhahabu wa Golden Pride imelipa kodi ya mapato ya Sh6.1 bilioni.
Dk Kayandabila anasema fedha hizo ni kodi ya mapato ambayo imefikisha jumla ya Sh97 bilioni tangu kampuni hiyo ilipoanza kulipa kodi ya mapato mwaka 2010.
Anasema kwa upande wa kampuni ya dhahabu ya Geita imelipa Sh4.8 bilioni na kufikisha jumla ya Sh304.2  bilioni tangu ilipoanza kulipa kodi ya mapato ya mwaka 2009.
Dk Kayandabila anasema kampuni ya almasi ya Williamson imelipia Sh178.9 milioni kama altenative minimum tax na  malipo hayo yalifanyika kwa mujibu wa sheria ya kodi ambayo inataka mlipa kodi  anayepata hasara kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kulipa aina hiyo ya kodi ambayo hutozwa kwa kukokotoa asilimia 0.3 ya mauzo ya kipindi husika.
Mgodi wa Tuwalawaka unaomilikiwa na ABG haukulipa kodi ya mapato katika kipindi hiki kutokana na mdororo wa bei ya dhahabu na mgodi huo ulifungwa rasmi Julai 30, mwaka huu. Jumla ya kodi ya mapato ambayo imewahi kulipwa na kampuni hiyo  wakati wa uhai wake ni Sh77.4 bilioni.
“Malipo mbalimbali yaliyoyolipwa serikalini na migodi baada ya kubainika kutolipwa. Ukaguzi uliofanywa na TMAA imefanikiwa kukusanya jumla ya Sh3.46 bilioni ambazo zimelipwa serikalini.
Baadhi ya wamiliki wa migodi mikubwa na ya kati iliyokaguliwa katika kipindi cha Mei hadi Novemba, 2012, malipo hayo yanajumuisha mrabaha, kodi ya zuio na nyingine stahiki,” anabainisha Dk Kayandabila. 
Anasema Serikali imepata mrabaha na takwimu sahihi za madini yanayozalishwa na migodi mikubwa nchini baada ya TMAA kufanya ukaguzi wa uzalishaji na mauzo kwenye migodi mikubwa ya dhahabu ya Geita, Golden Pride, Bulyanhulu, Buzwagi North Mara, Tulawaka na New Luika.
Anaeleza kwamba pia kaguzi zinaendelea kufanyika katika mgodi wa almasi wa Mwadui, mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mirerani
 
 
Source : mwananchi communication

No comments: